Karibu Thamani Academy
Ni vigumu sana kufuata Ndoto zako. Lakini, ni hatari zaidi kama utaacha kabisa. Safari ikiwa ngumu, haina maana hautafika.
Thamani Academy jukwaa maalumu kwa ajili ya kutoa Kozi, mafunzo na bidhaa mbalimbali za kidijitali zitakazokusaidia kuongeza Thamani zaidi katika Biashara na Maisha yako.
Kupitia Bidhaa za maarifa kutoka Thamani Academy, utaweza kuokoa pesa, muda, na kuepuka usumbufu unaoweza kuupata katika kutafuta maarifa sahihi yatakayokusaidia kukua na kufikia malengo yako.
Ni kwa namna gani Thamani Academy Itakusaidia?
Kama mwanafamilia wa Thamani Academy (Tengeneza Account yako Bure), utapata taarifa za kozi MPYA kila mwezi kuhusu Masomo muhimu yatakayokuongezea Thamani zaidi katika Biashara na Maisha yako.
Tunazo Makala, Vitabu, Kozi na Mafunzo katika nyanya zote muhimu:
- Maendeleo Binafsi
- Maudhui ya Biashara
- Masoko na Mauzo Kidijitali
- Kutengeneza Chapa (Brand) Imara
- Mahusiano
na nyingine nyingi.

Historia
Thamani Academy ni Jukwaa la Kidijitali lenye Malengo ya kuleta Mabadiliko chanya kwa mjasiriamali, mfanyabiashara na kila mtu mwenye nia ya kuongeza Thamani zaidi katika Maisha na Biashara yake.
Ilianzishwa rasmi na Ndugu Anselmo John (Coach Ansey) mwaka 2018. Ilianza kama ukurasa wa Instagram, ukiwa na lengo la kuongeza Thamani zaidi kwa kila mtu, katika eneo la Maendeleo Binafsi.
Kutoka na mahitaji, pamoja na mabadiliko ya teknolojia, sasa Thamani Academy imedhamiria kuwa Jukwaa muhimu litakalowakutanisha pamoja Wajasiriamali, wafanyabiashara, pamoja na watu binafsi, na kuwapa Elimu na Mafunzo yatakayowaongezea Thamani zaidi katika nyanja mbalimbali.

Dhamira
Dhamira yetu imejikita katika Maeneo makuu 3;
1. Kuelimisha jamii namna ya kuongeza Thamani katika Biashara na maisha yao kidijitali.
2. Kuwezesha jamii kupata maarifa kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
3. Kushawishi ubunifu na matumizi sahihi ya fursa za kidijitali katika kuboresha maisha.

Maono
Kutengeneza Mazingira rafiki kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na watu binafsi, ili waweze kuongeza Thamani katika Maisha yao na kupata Matokeo sahihi katika Biashara.
Mazingira rafiki tunayokusudia, ni yale yaliyojengwa kupitia:
Jamii sahihi itakayowaleta watu pamoja katika kujifunza.
Walimu sahihi watakaosidia kutimiza ndoto na Malengo ya wanafunzi wetu.
Kozi sahihi zitakazosaidia kupunguza au kuondoa kabisa ukali wa changamoto za kupata Elimu na Maarifa kidijitali.
Timu ya Wataalamu wetu

Coach Ansey
Mtaalamu wa Maudhui & MasokoKama unatafuta njia za kukusaidia kukabiliana na Changamoto za kufanya Biashara kidijitali, na kuongeza Thamani zaidi katika Biashara yako, bila shaka unahitaji Elimu, Ushauri na Mafunzo kutoka kwa Coach Ansey.

Ungependa Kuwa Sehemu ya Wataalamu wetu?
Tafadhari, endelea kusubiri. Tutatoa taarifa na Maelekezo zaidi.

Thank very much kwa kuanzishwa Thamani Academy. Personally, imenisaidia sana. Nilipita kwenye wakati mgumu sana. Nilikuwa very depressed, for sure nilikata tamaa sana. Niliona giza mbele yangu, lakini mara baada ya kuifahamu Thamani Academy, nilipata ushauri ulionivusha completely and I can say I’m doing well now. Niko vizuri sana na everything is well.
