Sera ya Faragha
Sera hii ya Faragha inatumika kwa matumizi yako ya www.thamaniacademy.com (“Tovuti”) inayomilikiwa na Thamani Academy International, matawi yake, na washirika wake (kwa pamoja “Thamani Academy”). Faragha yako ni muhimu sana kwetu. Tunatamani kufanya matumizi yako kwenye Tovuti yetu yawe yenye kukuridhisha zaidi, na tunatamani utumie taarifa, maarifa, bidhaa, na fursa tunazotoa kupitia Tovuti yetu kwa uaminifu zaidi.
Tumeandika Sera hii ya Faragha ili kuonyesha namna tunavyojali faragha na usalama wa Taarifa zako. Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi kampuni yetu inavyokusanya taarifa kutoka kwa watumiaji wote wa huduma tunazotoa kwenye tovuti au kupitia Tovuti (“Kozi” na “Bidhaa zetu”) – wale wanaopata baadhi ya Huduma zetu lakini hawana akaunti (“Wageni”) na wale ambao wanaweza kununua bidhaa na/au kulipa ada ya huduma ya kila mwezi katika tovuti yetu (“Wanachama”) – tunachofanya na taarifa tunazokusanya, na haki ambayo Wageni na Wanachama wanazo kuhusu kukusanya na kutumia taarifa hizo. Tunakuomba usome Sera hii ya Faragha kwa makini na Kuielewa vizuri.
Ikiwa una maswali au malalamiko kuhusu Sera yetu ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia faragha@thamaniacademy.com.
Kanuni za Faragha Kutoka Thamani Academy
Thamani Academy hufuata kanuni zifuatazo ili kulinda faragha yako:
- Hatukusanyi taarifa zozote zinazoweza kukutambulisha kibinafsi zaidi ya inavyohitajika;
- Tunatumia taarifa zako kwa madhumuni tunayobainisha katika Sera hii ya Faragha, isipokuwa pale unapokubali zitumike vinginevyo;
- Hatuweki au kuhifadhi taarifa zako ikiwa hazihitajiki tena; na
- Mbali na yale tunayobainisha katika Sera hii ya Faragha, hatutoi taarifa zako kwa washirika wengine nje ya wale watakaoainishwa.
Taarifa Tunazokusanya
Tunakusanya taarifa na maelezo binafsi kutoka kwako pale unapoomba maelezo kutoka kwetu, kujiandikisha ili kujiunga katika orodha yetu ya Barua pepe (Email List), kufungua akaunti, kushiriki katika matangazo na ofa zetu, kushiriki katika tafiti zetu mbalimbali, kutumia au kununua Bidhaa na Huduma zetu, kuwasiliana nasi kuhusu ununuzi wa bidhaa au huduma, kutuma barua pepe, kupiga simu au kuwasiliana nasi.
Ili uweze kuanza au kukamilisha manunuzi kutoka kwetu, tutaomba taarifa au maelezo mafupi kutoka kwako kwenye fomu yetu ya kufanya manunuzi, ikiwa ni pamoja na taarifa zako za mawasiliano (kama vile jina, barua pepe au namba yako ya simu) na maelezo ya njia unayotumia kulipia bidhaa au huduma (kama vile namba utakayotumia kufanya Malipo).
Ukinunua bidhaa au huduma kwa ajili ya mtu mwingine, tutakusanya pia jina na taarifa za mtu huyo ili tuweze kushughulikia malipo ya bidhaa yake. Unapotupatia maelezo haya tutayatumia tu kwa sababu mahususi kama itakavyobainishwa.
Wageni au Wanachama wanapopakua na kutumia Huduma za Thamani Academy kwenye simu zao za mkononi au kifaa kingine cha mawasiliano, Thamani Academy hukusanya maelezo na taarifa hizo, ikiwa ni pamoja na taarifa za eneo alilopo mtumiaji. Thamani Academy hutumia taarifa hizi ili kuboresha Bidhaa, Huduma na utendaji kazi wa Tovuti yetu.
Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Taarifa tunazokusanya zinaweza kutumika kwa njia zifuatazo:
- Ili kukutaarifu kuhusu marekebisho au maboresho ya Tovuti yetu, Bidhaa au Huduma zozote tunazotoa.
- Ili kujibu maombi au maswali yako.
- Ili kuchakata na kukamilisha malipo, ikijumuisha, huduma kwa wateja, kuwasilisha Bidhaa au Huduma, na vinginevyo kutimiza majukumu yetu ya kiutendaji ili uweze kufurahia huduma zetu.
- Ili kukupa majarida, makala, au programu, Bidhaa, au Huduma, taarifa na matangazo.
- Kufanya utafiti wa kimasoko kuhusu bidhaa au huduma zetu.
- Kuchanganua historia ya miamala na ununuzi ili kuboresha bidhaa, huduma, na programu nyingine.
- Inapohitajika ili kuthibitisha utambulisho wako.
- Ili kuweka rekodi za mawasiliano yetu na wewe ikiwa utaweka oda ya bidha au huduma zetu au kushughulika na wawakilishi wetu.
- Ili kuzuia, kuchunguza au kutoa taarifa ya ulaghai, shughuli zisizo halali au za uhalifu, au ufikiaji usioidhinishwa wa matumizi ya taarifa zinazomtambulisha mtu binafsi, Tovuti yetu au mifumo yetu ya taarifa.
- Kutekeleza wajibu wetu na kutekeleza haki zetu.
Haki zako
Una haki ya kuomba nakala ya taarifa binafsi ambayo tunaihifadhi kuhusu wewe. Ikiwa ungependa kupata nakala ya taarifa zako binafsi, tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia maelekezo ya mawasiliano hapa chini. Tunaweza kuomba uthibitisho wa utambulisho wako kabla ya kukutumia taarifa hizo. Ukigundua kuwa taarifa tulizonazo kuhusu wewe si sahihi au zimepitwa na wakati, unaweza kutuomba tusahihishe taarifa hizo kwa kututumia barua pepe kwenda faragha@thamaniacademy.com.
Katika mazingira flani (pale inapobidi ), unaweza kuomba tufute taarifa tunazohifadhi kuhusu wewe. Inaweza isiwezekane kwetu kufuta taarifa zako zote, hasa pale ambapo tunashughulikia manunuzi ya bidhaa au kuwa na sababu za msingi zinazotulazimu kuhifadhi taarifa hizo. Hata hivyo, tafadhali wasiliana nasi ili kujadili jinsi tunavyoweza kukusaidia zaidi.
Tafadhali, kama utakuwa na maswali zaidi kuhusu haki za taarifa zako, unaweza kutuma kwenda faragha@thamaniacademy.com.
Tutaendelea kuhifadhi taarifa zako endapo tu akaunti yako itakuwa hai au inavyohitajika ili kutimiza maombi yako, kukupa huduma au bidhaa, kutimiza majukumu yetu, kutatua changamoto na kutekeleza makubaliano yetu.
Kama hautopenda kupokea barua pepe kutoka kwetu kuhusu Bidhaa mpya au zilizopo Thamani Academy, Huduma na Ofa maalum kwa ajili yako, unaweza kujiondoa katika barua pepe zetu kwa kubofya “jiondoe/Unsubscribe” ndani ya kila barua pepe.
Vidakuzi (Cookies) na Teknolojia Nyingine za Ufuatiliaji
Kama ilivyo kwa Tovuti nyingi, tunakusanya baadhi ya taarifa na kuzihifadhi kwenye faili zetu za kumbukumbu. Taarifa hzii zinaweza kujumuisha anwani za itifaki ya mtandao (IP Adress), aina ya kivinjari/browser inayotumika, kurasa ulizoingia na kutoka ndani ya tovuti yetu, kurasa zinazotazamwa zaidi kwenye tovuti yetu, ili kuchanganua mienendo ya watumiaji wetu kwa ujumla na kusimamia tovuti yetu.
Thamani Academy hutumia vidakuzi/cookies au teknolojia kama hizo kuhifadhi taarifa, kuchanganua tabia na mienendo ya watumiaji, kusimamia Tovuti, kufuatilia mienendo ya watumiaji kwenye Tovuti, na kukusanya taarifa za idadi ya watumiaji wetu kwa ujumla.
Ufichuaji wa Taarifa Zako Binafsi
Utaratibu wetu kuhusiana na ufichuzi wa taarifa zako binafsi ni kama ifuatavyo:
Idhini. Tunaweza kufichua Taarifa zako binafsi kwa washirika wengine kwa idhini yako ya moja kwa moja. Taarifa zilizokusanywa kupitia SMS hazitatolewa kwa namna yoyote.
Washirika Kibiashara. Tunaweza kufichua taarifa zako binafsi kwa kampuni yetu kuu, washirika wetu kibiashara, na wakufunzi ambao unanunua bidhaa zao kupitia tovuti yetu, kwa matumizi yao kwa namna iliyoelezwa katika Sera ya Faragha.
Mawakala/Watoa Huduma. Tunatumia watoa huduma wengine kutusaidia katika kutoa Huduma na kuendesha Tovuti yetu, ikijumuisha watoa huduma wanaosimamia tovuti yetu ili kulinda taarifa zetu, na huduma za kuzuia udukuzi. Tunaweza kufichua taarifa zako binafsi kwa wahusika wanaotusaidia hukamilisha miamala, malipo au kufanya huduma kwa niaba yetu au kwa faida yako. Tunaweza kutumia huduma za wahusika wengine ili kuthibitisha taarifa ya mteja, au kuongezea taarifa nyingine tuliyokusanya. Tunaweza pia kuingia mkataba na wahusika wengine ili kuendesha Tovuti yetu na kufanya utafiti wa kimasoko. Watoa huduma wote wameidhinishwa kutumia taarifa zako binafsi inapohitajika tu, ili kutoa huduma zao kwetu, na wana wajibu wa kulinda taarifa zako chini ya masharti ya mkataba ambayo si kinyume na yale yaliyoainishwa katika Sera hii.
Mchakato wa Kisheria. Tunaweza kufichua taarifa zako binafsi kama itavyotakiwa na taratibu za kisheria, kama vile kutii wito au mchakato mwingine wa kisheria, au tunapoamini kwa nia njema kwamba kufichua ni muhimu ili kulinda haki zetu, kulinda usalama wako au usalama wa wengine, kuchunguza ulaghai, au kujibu ombi la serikali.
Uhamisho fulani wa Biashara. Taarifa zako binafsi zinaweza kufichuliwa kama sehemu ya shughuli za kibiashara, kama vile ubia, ufadhili au uuzaji wa mali ya Thamani Academy, na zinaweza kuhamishiwa kwa wahusika wengine kama moja ya mali ya biashara. Tutatumia juhudi zinazofaa kumuelekeza mhusika mwingine yeyote kutumia taarifa zako katika namna inayoheshimu Sera yetu ya Faragha.
Utapewa taarifa kupitia barua pepe na/au ujumbe maalumu kwenye Tovuti yetu kuhusu mabadiliko yoyote ya umiliki au matumizi ya taarifa zako.
Usalama
Usalama wa taarifa zako ni muhimu sana kwetu. Tunafuata viwango vinavyokubalika kwa ujumla ili kulinda taarifa zinazowasilishwa kwetu, wakati wa kujiunga na huduma zetu na mara tunapopokea taarifa husika. Katika uhalisia, hakuna njia ya uwasilishaji kupitia Mtandao, au njia ya uhifadhi wa kielektroniki, iliyo salama kwa 100%. Hata hivyo, wakati tunajitahidi kutumia njia zinazokubalika kibiashara kulinda taarifa zako, hatuwezi kukuhakikishia usalama wake kwa 100%. Taarifa tunazokusanya kuhusu wewe, huhifadhiwa katika seva zetu. Tunajitahidi kudumisha ulinzi ili kulinda usalama wa seva hizi na taarifa zako.
Tovuti za wahusika wengine
Tunaweza kuweka tovuti za wahusika wengine katika makala zetu mbalimbali. Ukibofya kwenye tovuti hizo, utaondoka kwenye tovuti yetu na kwenda kwenye tovuti uliyochagua. Kwa sababu hatuwezi kudhibiti shughuli za wahusika wengine, hatuwajibiki na matumizi yoyote ya taarifa zako kwa wahusika wengine, na hatuwezi kukuhakikishia kwamba watafuata desturi na sera za faragha kama sisi. Tunakuhimiza ukague sera za faragha za tovuti nyingine yoyote unayotembelea au mtoa huduma ambaye unaomba huduma kutoka kwake ili kujiweka katika mazingira salama zaidi.
Mabadiliko ya Sera hii ya Faragha
Tuna haki ya kurekebisha Sera hii ya Faragha wakati wowote. Ikiwa tutafanya mabadiliko muhimu kwa sera hii, tutakujulisha hapa, au kwa njia ya notisi kwenye Tovuti. Iwapo tutafanya mabadiliko yoyote makubwa kwa jinsi tunavyotumia taarifa zako, tutakujulisha kwa barua pepe. Utakuwa na fursa ya kuchagua kujitoa katika matumizi mapya au tofauti ya taarifa zako kabla ya mabadiliko kuanza kufanya kazi. Tunakuhimiza kupitia ukurasa huu mara kwa mara kwa taarifa mbalimbali kuhusu mabadiliko au maboresho ya sera yetu ya faragha.
Maelezo ya Mawasiliano
Ikiwa una maswali yoyote, maoni au wasiwasi kuhusu Sera yetu ya Faragha, unaweza kuwasiliana nasi kwa kuwasilisha swali lako kwetu kupitia:
https://thamaniacademy.com/mawasiliano
Ili kuwasiliana nasi kwa barua pepe au namba za simu, tafadhali tuma;
faragha@thamaniacademy.com
Simu: +255 753 163 067
Tafadhali wasiliana nasi kama una maswali, changamoto au maoni yoyote kuhusu huduma na Bidhaa zetu.