Sera ya Fidia na Malipo kutoka Thamani Academy
Kozi na Bidhaa zote za Thamani Academy hazina fidia au kurejesha pesa. Kutokana na muundo wa bidhaa kutoka Thamani Academy, ambazo nyingi zipo katika mfumo wa kidigtali, mteja hupokea faida ya moja kwa moja kutoka katika bidhaa husika baada tu ya kuinunua.
Si rahisi kurejeshwa kwa bidhaa kama vile maudhui yote ya kozi, vitabu, programu na nyenzo nyinginezo za kidijitali, kwa sababu mteja anakuwa tayari amepokea 90% ya bidhaa husika. Hivyo basi, jitahidi sana kuwa makini pale unapochagua bidhaa au kufanya uhakiki wa bidhaa kabla ya kukamilisha malipo.
Programu na Mafunzo ya ana kwa ana yanayotolewa na Thamani Academy, hayana fidia, isipokuwa pale inapotokea programu au mafunzo husika kugairishwa.
Iwapo una maswali yoyote kuhusu sera yetu ya fidia, tafadhali wasiliana na msaada@thamaniacademy.com