Ni mara ngapi umewahi kufanya Matangazo Instagram, lakini ukaishia kupoteza pesa zako bila kupata matokeo uliyotarajia? Katika uhalisia, sio kila tangazo utakalolifanya, linaweza kukupa matokeo mazuri katika mtandao wa Instagram, wenye watumiaji Zaidi ya 300M kila siku.
Lakini, hii isiwe sababu ya kukukatisha tamaa, kwa sababu katika makala hii utagundua Makosa 5 unayoyafanya katika Matangazo yako na njia zipi utumie ili kuhakikisha pesa yako haiendi bure.
KOSA #1: Unakosa malengo sahihi
Nimekutana na wafanyabiashara wengi sana. Ukiwauliza unataka kutimiza nini kupitia matangazo yako. Utasikia wanasema “Kupata Mauzo mengi”, “Kupata followers wengi” Inawezekana hata wewe umewahi kuweka malengo kama haya, right?
Ni malengo mazuri, lakini SIO SAHIHI kwa sababu hujawa specific, unataka kutimiza nini hasa katika mauzo au followers. Ukishindwa kuwa specific katika malengo au plan zako, basi unaasilimia kubwa sana ya kupoteza pesa yako katika matangazo.
Nini cha kufanya? Kuwa specific Zaidi katika malengo au plan zako
Kadri unavyokuwa specifi na aina ya matokeo unayotamani kuyapata kupitia tangazo lako, ndivyo unavyotengeneza nafasi ya kufanya vizuri. Vilevile, malengo unayoweka yanakusaidia kukupa muongozo wa namna ya kutengeneza tangazo lako na aina ya caption utakayoandika.
Mfano wa Malengo specific ni;
- Kuongeza watu 30 katika group lako la biashara
- Kuongeza Follower 20 kupitia tangazo hili
- Kupata wateja 5 ndani ya week hii
- Kuongeza awareness ya brand yako ili watu wakutambue Zaidi
- Kufanya mazungumzo na wateja 5 wapya
KOSA #2: Una Target kila mtu katika tangazo lako
Unaweza kuwa na Tangazo zuri, caption inayovutia, lakini bado usifanye vizuri kwa sababu ya kushindwa kutambua mtu uliyemlenga ili aweze kuona tangazo lako. Na hili linatokana na tamaa ya kutaka kumfikia kila mtu au kumuonyesha kila mtu tangazo lako.
Tangazo lolote linalomlenga kila mtu, siku zote halitamfikia mtu yeyote. Ndio hapo sasa, utaona unapata likes za kutosha tu, lakini huoni impact nyingine yoyote. Ni muhimu sana kuchagua kundi la watu unaotaka kuwafikishia ujumbe kuhusu tangazo, na wana nafasi ya kuchukua hatua endapo wataona ujumbe unaowagusa moja kwa moja.
Nini cha kufanya? Tengeneza Audience Tofauti tofauti kulingana na aina ya Tangazo lako
Instagram inakupa uwezo wa kutengeneza makundi mbalimbali ya Audience kila unapotaka kuweka tangazo. Wakati unatengeneza Tangazo utapewa option ya kuchagua “Create Audience” Mara nyingi, hawa ni audience waliofollow ukurasa wako au kufanya interaction na ukurasa au post zako kwa kiasi kikubwa.
Mbali na hii, unaweza kutengeneza list tofauti tofauti ya audience kulingana na malengo “Objetive” utakayoichagua wakati unatengeneza Tangazo lako. Hii itakusaidia kutambua ni Audience list ipi inakupa matokeo Zaidi kulinga na malengo uliyoyaweka kabla ya kufanya tangazo lako.
KOSA #3: Unatumia aina moja ya Tangazo
Yes! Lengo kubwa la mtandao wa Instagam wakati unaanzishwa, ilikuwa ni kushare picha. Kwa sababu hii, wafanyabiashara wengi ni kama wameingia kwenye kifungo cha mazoea, kwa kutumia mfumo wa picha tu katika kufanya matangazo. Hebu jitoe katika kifungo hicho, kwa kubadili ladha ya matangazo yako.
Nini cha kufanya? Chagua aina tofauti tofauti ya Matangazo
Sasa hivi, Instagram inakupa uwezo wa kufanya matangazo ya aina tofauti tofauti kulingana na mahitaji yako. Kila aina ya tangazo ina faida yake, hasa kuligana na malengo yako. Kikubwa, angalia malengo yako na matokeo unayotaka kutimiza, kabla ya kuchagua ni aina ipi ya tangazo unataka kufanya.
Hizi ni aina mbalimbali za matangazo unazoweza kufanya;
- Matangazo ya Picha.
- Matangazo ya Video:
- Matangazo ya picha Zaidi ya moja (Carousels):
- Matangazo kupitia Insta Stories.
- Matangazo kupitia Reels.
KOSA #4: Huna tabia ya kuangalia Data za maendeleo yako
Mtu wa kwanza kabisa unaeweza kujifunza kutoka kwake, ni wewe mwenyewe. Kufanya matangazo kwenye hii mitandao ya kijamii (Hasa Instagram), kuna faida kubwa sana, kwa sababu unapata nafasi ya kupima na kuangalia kila kitu unachokifanya katika account zako. Usifanye makosa ya kudharau kupitia data hizi, ambazo unazipata bure kabisa bila kulipia chochote.
Nini cha kufanya? Tumia vizuri Analytics Data unazopewa katika Account zako
Njia pekee ya kuangalia maendeleo ya Matangazo yako, na ukuaji wa ukurasa wako ni kutumia vyema;
- Instagram Insights
- Facebook Ad manager
KOSA #5: Hauzingatii kwa makini Location ya Tangazo lako
Eneo analoishi au kupatikana mteja wako u Audience uliyemlenga, linaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa matokeo ya Tangazo lako. Epuka kuchagua location yoyote, kwa sababu tu, unataka tangazo lako liende hewani.
Nini cha kufanya? Angalia location unayofatiliwa Zaidi
Siku zote, onyesha bidhaa yako mbele ya macho ya watu wanaotamani kuiona Zaidi. Unaweza kufahamu Top locations za Audience wanaokufatilia na kufahamu ni nchi au mikoa gani wanaongoza kukufatilia Zaidi, kwa kuangalia data zako katika Instagram Insights.
Pamoja na kwamba unaweza kufanya matangazo yako kwa haraka zaidi kupitia Instragram, unahitaji kuwa makini sana na kila hatua wakati wa kutengeneza Tangazo lako ili uweze kutegengeza mazingira rafiki ya kupata matokeo unayoyahiaji.