
Mitandao ya Kijamii ni moja ya eneo kiungo muhimu sana kama unataka kukua na kuendelea kusurvive kibiashara huku mtandaoni. Kama mfanyabiashara unaetumia au unapanga kutumia mitandao ya kijamii ili kutafuta wateja Zaidi, basi hakikisha unafahamu mambo muhimu yanayoweza kukusaidia kuchora barabara nzuri ya kufikia malengo yako.
Katika makala ya leo nitaenda kushare mambo 5 Muhimu sana kwako wewe mfanyabiashara kama unatamani kukuza Biashara yako Online. Namba 4 ni Muhimu sana, hakikisha unaifanyia kazi kila wakati.
Moja: Hakikisha unafahamu vizuri Audience wako/Wateja unaokusudia kuwafikia.
Ni kosa kubwa sana wewe kama ni mfanyabiashara na kushindwa kufahamu watu unaowalenga kwa ajili ya bidhaa au huduma yako.
Kazi kubwa ya Mitandao ya Kijamii ni kukusaidia kuifikisha biashara yako katika macho ya walaji wanaohitaji sana bidhaa au huduma yako, kushindwa kutambua ni nani unamlenga kulingana na biashara yako itakufanya uishi kwa matumaini ukiwa huna uhakikika kama kesho utapata wateja watakaonunua bidhaa zako au lah.
Kwa hiyo sasa, kabla ya kila kitu, kabla ya hata kufungua ukurasa wako na kuanza kupost, hakikisha kwanza unatambua unaenda kuwasiliana nan ani au ni nani unalenga kumfikia ilia one bidhaa zako na kununua.
Mbili: Wekeza katika Maudhui Bora Zaidi
Maudhui yako hayapaswi tu kuonyesha muonekano wa bidhaa au huduma zako, ni muhimu sana yawe na uwezo wa kumvutia Audience wako na kumshawishi aweze kuengage katika ukurasa wako. Ndio maana kuna faida kubwa sana ya kuweka aina nyingine ya maudhui kama vile nukuu/quotes, maswali, kuwaeliisha wateja wako, badala ya kila siku kupost picha za bidhaa zako pekee.
Katika ulimwengu wa sasa, kama hautengenezi engagement katika ukurasa wako, sio rahisi sana kuvutia wateja katika ukurasa wako. Usishangae kuona mtu anakata mauno huku akitangaza bidhaa yake, hahahaha simaanishi na wewe ufanye hivyo.
Kadri ambavyo engagement ya ukurasa wako kupitia maudhui yako inavyoongezeka, ndivyo ambavyo mashine za Instagram zitakavyokusaidia kupeleka maudhui yako kwa watu wengi Zaidi.
Tatu: Epuka kutelekeza wateja walionunua Bidhaa zako.
Miongoni mwa makosa makubwa yanayowafanywa na wafanyabiashara wengi, ni kuwatelekeza na kuwasahau kabisa wateja waliowahi kununua bidhaa kutoka kwao.
Nikuulize na wewe, mara yako ya mwisho kuwasiliana na wateja waliowahi kununua kutoka kwako ni lini?
Kazi ya mitandao ya kijamii sio tu kukusaidia kupata wateja wapya. Bali pia, kukusaidia kuwatunza wale ambao tayari wanafahamu kuhusu biashara yako na wamewahi kununua bidhaa zako. Kwa lugha rahisi, wana uzoefu na Bidhaa zako.
Jitahidi kujenga mahusiano na mawasiliano ya mara kwa mara na wateja wako. Hii itakakusadia sana pale unapohitaji kuwapa taarifa kuhusu bidhaa mpya , ofa, na discounts mbalimbali.
Epuka aibu na mfadhaiko usio na lazima. Usikae mwaka mzima bila kuwasiliana na wateja wako, halafu unasubiri siku za sikukuu au ukiwa na ofa au wakati mwingine ukiwa na njaa ya pesa, ndio uanze kuwatumia bidhaa zako. Watakutolea nje tu hahaha.
Nne: Usiache Kabisa Kufanya Matangazo.
Hebu fikiria,kama kila mfanyabiashara angelazimika kulipia matangazo katika Radio au Tv, wote tungeweza kumudu gharama zake?
Hii ndio faida kubwa ya mitandao ya kijamii, kukusaidia kufanya matangazo ya bidhaa zako kwa muda ana bajeti unayotaka wewe.
Lakini sasa, kuweka bajeti peke yake bado haitoshi, unapaswa kuhakikisha Tangazo lako linawafikia watu sahihi. Watu wanaoweza kununua bidhaa zako. Hapa sasa kuna umuhimu wa kufahamu jinsi ya kufanya matangazo kwa usahihi.
Kama unatamani kujifunza jinsi ya kufanya matangazo kwa usahihi, unaweza kupata kitabu hiki cha Instagram Ads au Kozi ya matangazo kutoka Thamani Academy. Nimeweka Link kwenye Description hapo chini.
Tano: Sio Dhambi kuomba Msaada.
Kamara wewe ni one – man army, jeshi la mtu mmoja, unaefanya kila kitu kuanzia kutafuta bidhaa, kuendesha kurasa zako na unajikuta una mrundikano wa mambo mengi kiasi kwamba unakosa muda wa kufocus na biashara yako kwa asilimia 100, basi sio dhambi kutafuta wataalamu wanaoweza kukusaidia kusimamia account zako, huku wewe ukiendelea na mambo mengine muhimu kuhusu biashara yako.
Kuteseka sio kipaji, na hakuna tuzo ya mtesekaji bora. Kubali kutafuta watu wanaoweza kukusaidia katika mambo yanayohitaji utaalamu Zaidi. Itakurahisishia sana katika ukuaji wa Biashara yako.
Mwisho kabisa, jitahidi sana kuwa updated na mabadiliko mbalimbali yanayofanyika katika account zako. Hata kama una idadi kubwa ya followers online, lakini kama utakuwa unapost maudhui au bidhaa zilizopitwa na wakati, watakukimbia na kukosa interest na account yako pamoja na bidhaa zako.