
Ukweli ni kwamba, kwa sasa Mitandao ya kijamii ina watu wengi sana wanaofanya Biashara kama yako. Kuna mamilioni ya wafanyabiashara, kama wewe,wanatafuta namna ya kutengeneza attention na kushawishi wateja kununua bidhaa au huduma zao.
Katika mazingira haya, ni rahisi sana kumezwa na ushindani na kushindwa kuonyesha Biashara yako kwa mbele ya macho ya wateja.
Hii ina maanisha kwamba, kama hauna mipango sahihi, unaweza kuendelea kupoteza mud ana pesa nyingi sana, na mwisho wa siku kuichukia kabisa mitandao ya kijamii.
Sasa, tuseme kwamba labda mitandao ya kijamii haina faida yoyote katika Biashara kwa sasa? Hapana! In fact, ndio eneo pekee linaloweza kukusaidia kukua kwa haraka na kuwafikia wateha wako kwa wakati.
Changamoto kubwa ni kwamba, ukiondoa kupost na kufanya boosting ya post za bidhaa, wafanyabiashara wengi wanakosa maarifa sahihi ya kutumia Mitandao ya kijamii. Wengi hawana strategy na bajeti maalumu kwa ajili ya kupata matokeo ya muda mrefu.
Katika makala ya leo, tutaangalia siri muhimu sana unazohitaji kuzifahamu ili kutengeneza bajeti sahihi ya kukupa matokeo katika matangazo yako.
- Tengeneza Malengo ya Tangazo lako.
Kabla ya kufanya Tangazo lako, unapaswa kutambua malengo unayotaka kutimiza au matokeo unayotaka kupata kupitia tangazo lako. Hebu jiulize, unataka Tangazo lako likupatie matokeo gani?
- Je, ni kupata followers?
- Je, ni kuwashawishi wateja kufika dukani kwako?
- Au unataka kuuza bidhaa au huduma zako?
Ukishatambua malengo yako, unaweza sasa kufikiria kuhusu bajeti utakayotumia ili kufikia malengo yako. Moja ya kosa kubwa unalolifanya, ni kudhani kwamba unahitaji bajeti kubwa sana ili uweze kupata matokeo. Lakini, ukweli ni kwamba, unaweza kupata matokeo mazuri hata katika bajeti ndogo kama tu utakuwa makini kuchagua aina ya matokeo unayotaka kuyapata.
2. Mfahamu mlengwa wa Tangazo lako. Huyu anaitwa “Target Audience”
- Unataka Tangazo lako limfikie nani?
- Mlengwa wa Tangazo lako ana tabia gani?
- Yuko interested na vitu gani vinavyoendana na bidhaa yako?
Ukimfahamu mlengwa wa Tangazo lako mapema, itakusaidia kutengeneza Tangazo litakalokidhi mahitaji yake. Hii itakupa nafasi ya kuonyesha Tangazo lako kwa watu sahihi na wenye uwezekano mkubwa wa kununua Bidhaa yako.
3. Chagua Platform sahihi kwa ajili ya Tangazo lako
Mitandao ya kijamii haifanani na kila mmoja una taratibu zake za kufanya matangazo kulingana na watumiaji wake. Kwa hiyo, sio kila mtandao unakufaa kwa ajili ya kutangaza Bidhaa au huduma zako.
Mfano: Kama wewe ni Kampuni, na unauza Bidhaa zako kwa Makampuni mengine ili na wao wakauze kwa wateja wao (Mode hii ya Biashara tunaiita B2B), mtandao wa Linkedln unaweza kukufaa zaidi kuliko Instagram au Facebook.
Lakini, kama bidhaa zako zinawalenga walaji moja kwa moja (Consumers) au wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo, basi Instagram na Facebook ni platform zinazokufaa. Muhimu ni kuhakikisha unachagua Platform inayoendana na Biashara yako, na wateja wako wawe ni watumiaji wakubwa wa platform hiyo.
4. Fahamu kiwango unachotaka kutumia katika Tangazo lako
- Unataka kutumia kiasi gani katika Tangazo lako?
Hii itategemea malengo yako, size ya Audience unaotaka kuwafikia, na platform utakayoichagua kwa ajili ya kuweka Tangazo lako.
Hata hivyo, sio lazima kutumia mtaji wako wote katika matangazo, bali unahitaji kuweka kiwango cha pesa kitakachokusaidia kufikia malengo uliyojiwekea. Hata kwa bajeti ndogo, bado unaweza kufikia malengo yako. Kadri, malengo yako yanavyoongezeka, basin a bajeti yako iongezeke pia.
Kutengeneza bajeti sahihi ya Matangazo yako ni jambo la msingi sana kama unataka kufikia wateja sahihi watakaonunua Bidhaa au Huduma zako.
Kwa kuchagua malengo sahihi, watu sahihi, na platform sahihi kwa ajili ya Tangazo lako, unaweza katika kutengeneza bajeti itakayokupa matokeo mazuri wakati wa kufanya Matangazo yako.