Utangulizi
Masharti haya ya matumizi hapa chini (“masharti”) yanasimamia matumizi yako ya tovuti yetu ya thamaniacademy.com (“tovuti”). Masharti haya ni mkataba wa kisheria kati yako na Thamani Academy International (“Thamani Academy”, au “sisi”), ambayo inasimamia matumizi yako ya huduma, bidhaa na maudhui yoyote tunayotoa kwenye tovuti au kupitia tovuti yetu. Kupitia Matumizi yako ya tovuti, huduma au bidhaa zetu, ina maana kwamba unakubali kutii kila masharti yaliyo hapa chini. Ikiwa hukubaliani na masharti haya, tafadhali usitumie tovuti hii, huduma au bidhaa zetu.
Thamani Academy hutoa Huduma, Maudhui na bidhaa katika tovuti ikiwalenga watumiaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18. Huduma tunazotoa kwenye tovuti au kupitia tovuti zinajumuisha, miongoni mwa bidhaa nyingine, utoaji wa kozi za moja kwa moja na zilizorekodiwa kuhusu mada mbalimbali. Taarifa zote, hati, bidhaa na huduma, ikiwa ni pamoja na kozi, nyenzo (Material) za kozi, maudhui, chapa za biashara, nembo, michoro na picha (ambazo kwa pamoja tunaziita “Nyenzo”) zinamilikiwa na Thamani Academy, au watoa leseni wake au wachangiaji, na matumizi yote ya Nyenzo hizi yako chini ya masharti haya.
Kozi za Thamani Academy na maudhui ya Kielimu kuhusu Biashara mtandaoni ni ya dijitali na yanapatikana mara moja unapojiandikisha kama mwanachama wa thamaniacademy.com na kukamilika kwa malipo. Hakuna usafirishaji wowote wa bidhaa nje ya tovuti yetu..
Kwa kufanya uamuzi wa KUTUMIA TOVUTI YETU, UNAKUBALI KUFUATA na kutekeleza Taratibu na maelekezo haya;
1. Sera ya Faragha
Maelezo na Taarifa tunazokusanya kwenye tovuti yanasimamiwa na Sera ya Faragha ya thamaniacademy.com, ambayo inapatikana kwenye tovuti hii kwenye ukurasa wetu wa Sera ya Faragha . Sera ya Faragha ni sehemu ya masharti haya na inajumuishwa katika sheria na masharti haya kwa marejeleo.
2. Maboresho ya Sheria na Masharti haya na Huduma za Thamani Academy.
Thamani Academy inaweza kubadili sheria na masharti haya kama sehemu ya kufanya mabadiliko kwenye tovuti, huduma au bidhaa zetu, na Thamani Academy ina haki ya kurekebisha na/au kufanya mabadiliko ya sheria na masharti haya wakati wowote. Iwapo Thamani Academy itafanya mabadiliko yoyote ya masharti haya, tutakujulisha kwa kutumia notisi ya barua pepe itakayotumwa kwa anwani ya barua pepe iliyounganishwa na akaunti yako au kwa kutuma notisi kwenye tovuti, na wakati mwingine kupitia Kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii. Mabadiliko yoyote yataanza kutumika siku ambayo yatachapishwa, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo.
Ikiwa utaendelea kutumia tovuti baada ya mabadiliko hayo kuchapishwa, inamaanisha kuwa unakubali sheria na masharti mapya, hata kama hujakagua na kuangalia mabadiliko yaliyofanyika. Tafadhali, jitahidi sana kuangalia sheria na masharti haya mara kwa mara.
Thamani Academy inaweza kurekebisha tovuti, Nyenzo (Material), Maudhui, huduma na bidhaa, au kukomesha matumizi au upatikanaji wa hayo yote wakati wowote.
3. Usajili wa Akaunti
Ili uweze kutumia Nyenzo (Material), bidhaa au huduma yoyote kwenye tovuti, utahitaji kujiandikisha kwa kufungua akaunti. Unapojiandikisha, utahitaji kutoa taarifa fupi kama vile jina lako, barua pepe na nenosiri. Una jukumu la kudumisha usiri wa akaunti na nenosiri lako (kwa pamoja, “akaunti yako”) na kulinda shughuli zote zinazohusiana na/au zinazofanyika chini ya akaunti yako. Unawajibika kuthibitisha kwamba, maelezo ya akaunti yako yatakuwa sahihi wakati wote. Ni muhimu umjulishe Thamani Academy Admin mara moja ikiwa utafahamu matumizi yoyote yasiyoidhinishwa ya akaunti yako au ukiukaji wowote wa usalama wa akaunti yako. Unawajibika kwa hasara au uharibifu wowote unaotokana na kushindwa kwako kuzingatia usiri na uhifadhi wa akaunti yako na kwa vitendo vyote vinavyotokea kuhusiana na akaunti yako, iwe ni kwa kufahamu au bila kufahamu, kabla ya kumjulisha Thamani Academy Admin juu ya matumizi yoyote yasiyoidhinishwa ya akaunti yako. Hauruhusiwi kuhamisha akaunti yako kwa mtu mwingine yeyote au kutumia akaunti ya mtu mwingine ili kupata Huduma za Thamani Academy.
4. Leseni au Ruhusa ya Matumizi ya Huduma
Thamani Academy itakupa leseni ndogo (binafsi) isiyoweza kuhamishwa kwa ajili ya kutumia tovuti na Nyenzo (Material) zake, ikijumuisha kozi na maudhui ambayo umelipa ada, kwa matumizi yako binafsi, au ya kielimu pekee. Unakubali kwamba utatumia tovuti na Nyenzo zake kwa mujibu wa masharti haya.
Unakubali kuwa huna haki ya kurekebisha, kuhariri, kunakili, kuzalisha tena, kusambaza, kuuza, kukodisha, kukopesha, kushiriki katika kubadilisha, kuboresha au kwa njia yoyote kutumia Nyenzo yoyote iliyotolewa na Thamani Academy kwa njia yoyote bila ruhusu na Taarifa maalumu. Leseni yako ndogo ya kufikia tovuti na kutumia Nyenzo zetu inaweza kusitishwa mara moja, bila kutoa taarifa kwako, ikiwa utakiuka mojawapo ya masharti haya.
Baada ya kusitishwa kwa leseni yako, unakubali kufuta mara moja bidhaa na nyenzo zote zilizopakuliwa (Download) au zilizochapishwa kutoka Thamani Academy. Isipokuwa kama ilivyoelezwa hapa, unakubali kwamba huna haki, ya kutumia jina au taarifa zako tena katika tovuti au Nyenzo yoyote.
5. Malipo na Ada ya Huduma au Bidhaa
Unawajibika kikamilifu kwa huduma zote, ada za huduma na/au gharama zingine zinazohusiana na matumizi yako ya tovuti, kozi, bidhaa na Nyenzo zake kadri itakavyoonyeshwa katika kila bidhaa au huduma.
Ukichagua kutumia bidhaa, kozi au Nyenzo yoyote, au kujiandikisha kwa ajili ya usajili wa kozi au huduma ambayo inahusisha malipo ya ada, unakubali kuwajibika kwa malipo yote yanazohusiana na bidhaa au Huduma hiyo. Ikiwa utatoa maelezo au taarifa za kadi ya malipo ili kulipia ada kama hizo, unawakilisha na kuthibitisha kwamba umeidhinishwa kutoa taarifa au maelezo hayo ya malipo na kuidhinisha Thamani Academy kutoza kadi yako ya malipo mara moja au mara kwa mara, kadri inavyotumika wakati wa kufanya malipo.
Kwa usajili unaolipishwa (Subscription), Thamani Academy itapokea na kuhifadhi usajili wako kiotomatiki na kutoza kadi yako ya malipo. Ada ya kufanya maboresho ya huduma hii itakuwa sawa na ada ya usajili inayotumika katika huduma husika toka mwanzo, isipokuwa kama Thamani Academy itakupa angalau siku 30 kabla ya notisi ya maandishi ya ongezeko la ada, ambayo itaanza kutumika baada ya maboresho kufanyika. Ada za kozi au huduma zingine zitatozwa kulingana na gharama ya bidhaa husika.
Iwapo njia yako ya kufanya malipo itakwama au akaunti yako haijalipiwa, Thamani Academy inaweza kukusanya ada zinazodaiwa kwa kutumia mbinu nyingine za kufanya malipo, kama vile Lipa Namba, Bank au kutumia njia nyingine za malipo zitakazoidhinishwa na Thamani Academy. Tunaweza pia kuzuia matumizi yako ya kozi au Nyenzo zozote zinazosubiri malipo ya kiasi chochote kutoka kwako kwenda Thamani Academy.
6. Matumizi ya Tovuti na Nyenzo zake
Matumizi yako ya Tovuti na Nyenzo zake, bidhaa na huduma, unategemea sana namna utakavyofuata sheria na masharti haya. Bila kubadili yale tuliyoainisha hapo juu, unakubali kutofanya hivi:
▶ Kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu au kuzuia utendaji wa miundombinu ya tovuti;
▶Kujaribu kuharibu kwa makusudi tovuti na/au bidhaa au huduma zozote zinazotolewa kwenye tovuti kwa kutumia virusi vya kompyuta au programu au msimbo wowote unaokusudiwa kutatiza au kuzima utendakazi wa tovuti na/au ufikiaji wa Nyenzo zake;
▶Kutumia roboti au programu nyingine kubadili sehemu yoyote ya tovuti ya Thamani Academy;
▶Kuiba au vinginevyo kukusanya taarifa kuhusu watumiaji wengine kwa madhumuni yoyote isipokuwa kama inavyoruhusiwa hapa;
▶Kuchapisha taarifa au maelezo yoyote ya uongo au yasiyo sahihi (yaliyofafanuliwa hapa chini) au habari kwenye sehemu yoyote ya tovuti;
▶Kutumia Nyenzo na/au tovuti kuvunja sheria au kanuni zozote zinazotumika, ikijumuisha, ukiukaji wa hakimiliki yoyote, chapa ya biashara, au haki nyinginezo za kiubunifu, au kukiuka faragha au haki za mtu mwingine yeyote katika tovuti;
▶Kuchapisha taarifa au maelezo yenye viashiria vya kibaguzi, chuki, matusi, kashfa, yenye mwelekeo wa kingono, vitisho, au vingine visivyofaa;
▶Kunyanyasa, au vinginevyo kumdhuru mtumiaji mwingine yeyote wa tovuti au Nyenzo zake kwa mawasiliano yasiyofaa au yasiyotakikana;
▶Kufanya nyongeza yoyote, mabadiliko, na/au kufuta maelezo au mawazo yoyote yaliyotumwa na mtumiaji mwingine (Hasa katika Comments na Review za Bidhaa zetu) bila idhini ya maandishi ya mtumiaji huyo;
▶Thamani Academy inahifadhi haki ya kusitisha uhusiano wetu na wewe chini ya masharti haya na kukataza matumizi yako ya tovuti na Nyenzo zake, kuondoa au kufunga moja kwa moja akaunti yako katika tovuti yetu.
Orodha hii ya makatazo haikusudiwi kuwa ndio mwisho wake. Thamani Academy inaweza kuongeza kwenye orodha hii wakati wowote, pale inapoona inafaa kufanya hivyo.
Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali kwamba unaweza kuonyeshwa maudhui ambayo yanaweza kukukera, kukuchukiza au kwenda kinyume na hisia au mtazamo wako. Matumizi yako ya tovuti na Nyenzo zake unafanywa kwa hiari yako mwenyewe na Thamani Academy haiwajibikii nyenzo au maudhui yoyote ambayo yanaweza kuchapishwa kwenye tovuti endapo yatakinzana na hisia au mtazamo wako binafsi.
Huruhusiwi kukwepa au kujaribu kukwepa udhibiti wa usalama unaotekelezwa na Thamani Academy ili kulinda tovuti, Nyenzo, bidhaa na taarifa yoyote unayotoa kupitia tovuti. Matendo mengine yanayopigwa marufuku yanajumuisha; (a) kuingia katika akaunti na nenosiri ambalo hujapewa; (b) kufikia maelezo au taarifa binafsi ambazo kwa njia za ulaghai; (c) kupima hatua za usalama kwenye tovuti na/au kujaribu kutambua udhaifu wa mfumo katika tovuti; (d) kuiga mtumiaji mwingine yeyote wa tovuti na/au bidhaa na huduma, kughushi taarifa yoyote; (d) kurekebisha, kubadilisha muundo, kutenganisha, au kujaribu vinginevyo kuruhusu watu wengine kujaribu kuharibu mfumo wa programu ya tovuti na/au bidhaa na huduma; au (f) kushiriki katika kuzima tovuti au bidhaa na huduma au kuingilia kati ufikiaji na matumizi ya tovuti na/au huduma ya mtumiaji mwingine yeyote.
Ikiwa tutafahamu shughuli zozote zilizo hapo juu au tabia nyingine iliyopigwa marufuku au kinyume cha sheria kwenye tovuti, tunaweza kuchunguza na kuchukua hatua. Inapofaa, tunaweza kufanya kazi na vyombo vya sheria kuchunguza na kuwashtaki wakosaji.
7. Mawasilisho ya Mtumiaji
Ukiwasilisha data na/au kuchapisha mawasiliano yako kwenye tovuti (“mawasilisho”), unairuhusu Thamani Academy kuchukua haki isiyoweza kubatilishwa, ya kudumu, isiyo na mrabaha, na kutoa ruhusa ya kutumia, kuonyesha, kusambaza, kurekebisha. na kutengeneza maudhui yanayotokana na mawasilisho hayo sasa au baadaye. Unadhibitisha kwamba taarifa zako ni sahihi, na hakuna mhusika mwingine ambaye amehifadhi au kutumia taarifa zako.
8. Notisi ya Hakimiliki
Nyenzo zote, bidhaa na Maudhui yanayotolewa kwenye tovuti ikiwa ni pamoja na kurasa za tovuti, nyaraka, muundo wa tovuti, maandishi, michoro, nembo, picha na icons mbalimbali na mpangilio wake, ni mali ya Thamani Academy, isipokuwa vinginevyo. Bidhaa zote zinalindwa na hakimiliki na sheria zinazotumika na kutolewa na Mamlaka husika.
Haki zote ambazo hazijatolewa waziwazi katika masharti haya zimehifadhiwa. Ni marufuku utoaji wowote, usambazaji, urekebishaji, utumaji upya, au uchapishaji wa bidhaa, maudhui au nyenzo zozote zilizo na hakimiliki kwenye tovuti bila idhini ya maandishi kutoka Thamani Academy, isipokuwa kama inavyotakiwa na sheria inayotumika.
9. Kuzingatia Sheria
Matumizi yako na shughuli zingine zinazohusiana na bidhaa na huduma zetu lazima zifuate sheria na kanuni zote zinazotumika, ikijumuisha, sheria zinazohusiana na hakimiliki na haki zingine za faragha, matumizi mazuri ya mtandaoni na maudhui yanayokubalika. Zaidi ya hayo, matumizi ya tovuti na huduma zake kinyume cha sheria ni marufuku na hatutaweza kuvumilia ukiukwaji wowote wa taratibu zilizoanishwa hapa.
10. Kukomesha Matumizi ya Huduma
Ikiwa utakiuka masharti haya, Thamani Academy inaweza kusitisha fursa ya kutumia tovuti au sehemu fulani za tovuti bila taarifa. Ingawa Thamani Academy inaweza kutoa nafasi ya kukushauri juu ya tabia yako isiyofaa na kupendekeza hatua yoyote muhimu ya kurekebisha pale ulipokosea. Muendelezo wa ukiukaji wa masharti haya, itasababisha kusitishwa mara moja kwa matumizi yako ya tovuti au sehemu fulani za tovuti. . Thamani Academy inahifadhi haki ya kusitisha akaunti yoyote kwa sababu yoyote.
11. Utatuzi wa Migogoro
Iwapo haujaridhika na tovuti, Nyenzo au ununuzi ambao umefanya kupitia tovuti, tafadhali wasiliana nasi kwa support@thamaniacademy.com ili tuweze kushughulikia suala lako. Iwapo hatujaweza kutatua malalamiko yako, mchakato ufuatao utatumika.
Mzozo wowote au madai yanayohusiana kwa njia yoyote na matumizi yako ya tovuti au Nyenzo yatatatuliwa kwa kupitia mazungumzo, badala ya mahakamani.
Kila mmoja wetu anakubali kwamba taratibu zozote za utatuzi wa migogoro zitaendeshwa kwa misingi ya ya mazungumzo kati ya Thamani Academy na wewe mtumiaji wa bidhaa au huduma zetu na sio muwakilishi. Iwapo kwa sababu yoyote dai au mgogoro utafika mahakamani kila mmoja wetu anapewa haki muhimu ya kusikilizwa. Sisi pia tunakubali kwamba wewe au sisi tunaweza kuwasilisha kesi mahakamani kuamuru ukiukaji au matumizi mengine mabaya ya haki miliki.
12. Masharti ya Jumla
Upungufu. Iwapo kifungu chochote cha masharti haya kitapatikana kuwa na mapungufu au hakitekelezeki, basi kifungu hicho kitachukuliwa kuwa kinaweza kutenganishwa na masharti haya na hakitaathiri uhalali na utekelezaji wa masharti yoyote yaliyosalia.
Taarifa. Notisi yoyote, taarifa au mawasiliano mengine yatakayotolewa hapa yataandikwa na kutolewa kwa njia ya barua pepe au kurasa zetu za mitandao ya kijamii.
Maelezo ya Mawasiliano. Ikiwa una maswali au maoni yoyote kuhusu huduma na Bidhaa zetu, tafadhali wasiliana nasi kwa:
Simu/Whatsapp: +255 753 163 067
support@thamaniacademy.com